Habari
MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA NA SHIRIKISHO LA FILAMU

Tarehe 20 Mei, 2022 Bodi ya Filamu Tanzania imetoa mafunzo maalum ya "USIMAMIZI WA FEDHA" na "UTAWALA/UONGOZI BORA" kwa Viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na Viongozi wa Vyama 9 vinavyounda Shirikisho hilo.
Lengo la mafunzo hayo ni kuongeza weledi, ufanisi na maarifa katika utendaji kazi wa Viongozi kwenye maeneo ya Fedha na Utawala.
Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Wataalam katona Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Bw. Omar Mtwenye (usimamizi wa fedha) na Bw. Haji Bakula (utawala bora).