Habari
KWAHERI

Serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania imeshiriki katika mazishi ya aliyekuwa mdau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uandaaji wa Filamu na Tamthilia ya Jasons Production Bw. Sanctus Mtsimbe, ambapo Misa ya kumuaga Marehemu imefanyika katika Kanisa la Waadventista Wasabato Tabata Segerea na Mazishi yamefanyika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Saalam.