emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​KONGAMANO LA WADAU WA FILAMU


Kuelekea kilele cha Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2023, Bodi ya Filamu Tanzania imeratibu Kongamano la wadau wa Filamu lililolenga kujadili namna mbalimbali za usambazaji wa Filamu za Kitanzania katika Soko la ndani na la kimataifa.

Kongamano hilo lililofanyika tarehe 15.12.2023 katika ukumbi wa Makao Makuu ya CRDB jijini Dar es Salaam, lilihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchini wakiwemo waanzilishi na Waratibu wa Tuzo za Kimataifa za Hollywood and African Prestigious (HAPAwards) za Hollywood, Marekani Bi. Tina Weisinger na Bi. Amberr Washington ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumza kuhusu nia yao ya kushirikiana na wadau wa Filamu nchini katika kutangaza Filamu za Kitanzania.