Habari
HAPAwards WATEMBELEA BODI YA FILAMU
Waandaaji na Waratibu wa Tuzo za Kimataifa za Hollywood and African Prestigious (HAPAwards) za Hollywood, Marekani Bi. Tina Weisinger na Bi. Amberr Washington, Oktoba 9, 2023 wametembelea ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania na kukutana na Katibu Mtendaji Dkt. Kiagho Kilonzo na pamoja Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu Bw. Emmanuel Ndumukwa kwa lengo la kuifahamu Taasisi hiyo kufuatia ziara ya Katibu Mtendaji kwenye Tuzo hizo zilizofanyika Hollywood, Marekani mapema Oktoba.