emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​HAFLA YA KUWAPONGEZA WASHINDI WA TUZO MBALIMBALI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa amewapongeza Wadau wa Sekta ya Sanaa na burudani nchini waliofanikiwa kushinda Tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi hivi karibuni wakiwemo Wasanii wa Filamu, Muziki, Watangazaji, Waandishi wa Vitabu, pamoja na wasimamizi wa Wasanii (Managers).

Pongezi hizo amezitoa katika hafla iliyofanyika tarehe 22 Novemba, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine ametoa Rai kwa wadau hao kutumia fursa ya Sanaa kutangaza nchi na kukuza vipato vyao.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Wakurugenzi kutoka Wizarani (USM), Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Watumishi wa Taasisi hizo, pamoja na Maraisi wa Mashirikisho ya Sanaa.