emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

GERSON MSIGWA ATAKA TAASISI ZA WIZARA KUSHIRIKIANA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa akiendesha kikao cha Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi kutoka kwenye Wizara hiyo.

Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 22 Novemba, 2023, pamoja na mambo mengine kimejadili kuhusu Mkakati wa Maendeleo ya Kisekta na namna sahihi ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo ili kukuza na kutangaza Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ndani na nje ya nchi.