emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

GABO NA WOLPER MABALOZI WAPYA WA BODI YA FILAMU


Bodi ya Filamu Tanzania May 19, 2023 imesaini hati ya makubaliano na Waigizaji Salim Ahmed maarufu na Jackline Wolper ya kuwa Mabalozi mapya wa Bodi hiyo lengo likiwa ni kuwafikia Watu wengi zaidi na kutangaza shughuli mbalimbali za Bodi.

Mabalozi hao watakuwa na jukumu la kutangaza shughuli za Bodi hiyo pamoja na kuhamasisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Sekta ya Filamu nchini.

Gabo na Wolper wanaungana na Balozi Kiongozi Yvonne Cherrie maarufu Monalisa ambaye tayari alitangazwa kuwa Balozi wa Bodi ya Filamu kuanzia Mwaka 2022.

Akiongea baada ya makubaliano hayo, Jackline Wolper ameahidi kutumia nafasi ya ubalozi kwa kuifanya Bodi na shughuli zake kujulikana ndani na nje ya Nchi kutokana na ushawishi wake kwenye Jamii.