Habari
FILAMU MTAA KWA MTAA MJINI TANGA

Tarehe 20 Mei, 2023 Maafisa wa Bodi ya Filamu wakiongozwa na Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo wakiwa katika programu ya Filamu Mtaa kwa mtaa, waliwatembelea Waandaji wa Filamu ya TANGAMANO, inayoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Ginniver Great Film na One Power Media, katika Mtaa wa Kisosora Kata ya Chumbageni jijini Tanga.