Habari
FILAMU MTAA KWA MTAA
Katika kuendelea kuwafikia wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini, wataalamu wa Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania wametembelea kambi ya waandaaji wa Tamthilia za mitandaoni hususan YouTube 'Bichwa Production' iliyopo Kisarawe Mkoa wa Pwani. Pamoja na mambo mengine, waandaji hao wamepewa elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo umuhimu wa vitambulisho vya wadau wa Filamu vinavyotolewa na Bodi ya Filamu.