Habari
BODI YATEMBELEA MAKTABA ZA VIDEO - TANGA
Katika muendelezo wa ziara ya Bodi ya Filamu jijini Tanga, tarehe 19 Mei, 2023 Maafisa Maendeleo ya Filamu Bw. Nathan Malaki na Bi. Boppe Kyungu wametembelea maeneo mbalimbali jijini humo na kukutana na wadau wa Maktaba za video kwa lengo la kuwapa elimu kuhusu urasimishaji wa shughuli za Filamu wanazozifanya.
Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa Leseni za kuendesha biashara hiyo, ambapo gharama ya Leseni kwa mwaka ni Shilingi za Kitanzania 36,000.00
Aidha, zoezi la kutoa elimu ya urasimishaji wa Maktaba za Video ni la muendelezo Nchi nzima. Bodi inatoa rai kwa Wamiliki wote wa Maktaba hizo kufuata utaratibu wa Kisheria unaowataka kuwa na Leseni ya uendeshaji wa shughuli hiyo.