emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU YATOA MAFUNZO TASUBA


Katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Bodi ya Filamu Tanzania imeratibu na kutoa mafunzo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kwa lengo la kuwapa uelewa kuhusu Bodi hiyo pamoja na masuala mbalimbali ya Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Katika mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo, pamoja na mambo mengine ameeleza hatua mbalimbali ambazo Bodi inazifanya katika kuimarisha Sekta ya Filamu ikiwemo: -

1. Kuratibu uandaaji wa Filamu mbalimbali za Kimkakati,

2. Kutoa mafunzo kwa Wadau wa Filamu,

3. Kuimarisha Taasisi za wadau ikiwemo vyama na Shirikisho la Filamu,

4. Kuratibu Kamati ya kulinda na kutetea haki za wasanii,

5. Kuratibu na kutoa Tuzo za Filamu ambapo kupitia Tuzo hizo wadau mbalimbali wamehamasika kuanzisha Tuzo zao zenye lengo la kuchochea na kuhamasisha Maendeleo ya Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.