emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​BODI YA FILAMU YATETA NA WADAU WA FILAMU TANGA


Katika kuwafikia Wadau wa Filamu nchini, tarehe 18 Mei, 2023 Bodi ya Filamu Tanzania imekutana na wadau wa Filamu wa jiji la Tanga kwenye kikao kazi cha kutoa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi ikiwemo umuhimu wa vibali vya Uandaaji wa Filamu/Tamthilia, Vitambulisho, pamoja na Leseni kwa wadau wa Filamu.

Pamoja na mambo mengine, Maafisa Filamu kutoka Bodi Bw. Nathan Malaki na Bi. Boppe Kyungu walitoa elimu kuhusu uandaaji wa kazi zenye kulinda maadili ya Kitanzania na kukemea uoneshaji wa Filamu zisizo na maadili kwenye Vibanda umiza ambavyo watoto wamekuwa wakiingia kutazama Filamu.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Muandishi wa miswada na Muongozaji Nguli wa Filamu ya The Green Tanzanite, Bw. Ignas Mkindi, ambapo aliwashirikisha wadau wa Tanga uzoefu wake katika Sekta ya Filamu. Aidha, aliwahamasisha kuhudhuria katika Uzinduzi wa Filamu ya The green Tanzanite, tarehe 20 Mei, katika ukumbi wa Majestic Cinema.