emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU YATETA


Katika muendelezo wa kutafuta wawekezaji wa Miradi mbalimbali inayoratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania, tarehe 25 Machi, 2024 Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo alikutana na Mabalozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Balozi Saidi Yakubu na Balozi John Ulanga.

Aidha, Katibu Mtendaji aliwapitisha katika baadhi ya miradi ikiwemo Mradi wa Eneo Changamani la Uandaaji wa Filamu na Mradi wa Akademia ya Filamu, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili kuhusu namna bora zaidi ya kufungua milango ya utafutaji Fedha za uwekezaji kutoka kwa wawekezaji Duniani.