emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU TANZANIA YATOA SOMO KWA WIZARA YA TEHAMA YA UGANDA


Tarehe1 Disemba, 2022 Bodi ya Filamu Tanzania ikiongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Kiagho Kilonzo imekutana na Jopo la Wataalam kutoka Wizara ya Tehama ya Uganda lililoongozwa na Waziri Mhe. Godfrey Baluku Kabbyanga.

Jopo hilo limetembelea Bodi ya Filamu kwa lengo la kujifunza namna Bodi inavyofanya kazi katika kuongoza Sekta nzima ya Filamu nchini, ili kutumia weledi huo kuboresha utendaji wao katika Sekta ya Filamu nchini Uganda.