emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​BODI YA FILAMU KUSHIRIKIANA NA JUKWAA LA "SOSHONAMIMI" KUTOA ELIMU KWA WADAU WA FILAMU


Akiongea katika mkutanao na Waandishi wa Habari Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo ameeleza kuwa nia ya Serikali ni kuongeza weledi kwa wadau wa Filamu nchini, ambapo tarehe 29 Aprili, 2023 Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Jukwaa la "SOSHONAMIMI" itaratibu Kongamano la wadau wa Filamu lenye lengo la kutoa elimu ya masoko ya Filamu Kidijitali.

Kongamano hilo ni muendelezo wa Kongamano lililofanyika tarehe 22 Mei, 2022 ambapo moja ya hoja zilizojadiliwa ilikuwa ni masoko na ununuzi wa Filamu katika Mitandao.

Jukwaa la "SOSHONAMIMI" lilianzishwa na Muigizaji Saida Khalfan almaarufu "Shadee" kwa lengo la kutoa elimu kwa vijana katika matumizi sahihi ya Mitandao ya Kijamii ambapo kwa mwaka huu linashirikiana na Bodi kwakuwa vijana ni moja ya kundi linalounda wadau wa Tasnia ya Filamu.