emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Dr. Kiagho Kilonzo

News Image
KIAGHO BUKHETI KILONZO ni mhitimu wa Shahada ya Uzamilivu aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2014, ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania kuanzia mwaka 2021, ambapo alikaimu nafasi hiyo tangu Mei, 2019. Dkt. Kilonzo alizaliwa mwaka 1976 Muheza, Tanzania. Dkt. Kilonzo alihitimu Shahada ya Uzamili wa Sanaa na Teknolojia katika Chuo Kikuu cha Texas Dallas na Shahada ya Sanaa ya Uchoraji katika Chuo Kikuu cha North Texas, USA baada ya kuhitimu Stashahada ya Sanaa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo Tanzania. Kabla ya wadhifa huu, alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania kabla ya uteuzi wake mwaka 2019. Mbali na uteuzi huo Dkt. Kilonzo alikuwa akifundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 2008 hadi 2019 na alikuwa mtahini wa nje katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA) mwaka 2017. Kwa muda wake wa ziada Dkt. Kilonzo alikuwa akijitolea kama Mtendaji Mkuu wa East Africa Art Biennale Association, taasisi inayojihusisha na kuibua wasanii wa Afrika Mashariki kwa kuandaaa maonesho kila baada ya miaka miwili kwa miaka saba (2013-2019), na Raisi wa Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya Jumuiya ya Kimataifa ya Sanaa (2010 hadi 2012). Pia katika Chuo Kikuu cha Dar es salam alikuwa Msimamizi wa Idara ya Mafunzo kwa Vitendo, Afisa Udhibiti wa Ubora wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Afisa Uhakiki wa Ubora wa Idara ya Insia Bunifu (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam), na alikuwa Mwenyekiti wa timu ya kufufua jarida la Ndaki ya Insia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dkt. Kilonzo ameshiriki mikutano mbalimbali ya ndani na kimataifa pamoja na uwasilishaji wa maandiko ya kitaaluma, warsha, matamasha ndani ya Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda, Nigeria, Senegal, Kenya, Afrika Kusini, China, Sweden and Uingereza. Dkt. Kilonzo alikuwa mshindi wa 3 katika shindano la Ndaki ya Insia (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) kwenye wiki ya utafiti wa chuo msimu wa mwaka 2017-2018.