emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Abdillah Amanzi

News Image
ABDILLAH AMANZI ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala mwaka 2012, ni meneja wa Utawala na rasilimali watu katika taasisi ya Bodi ya Filamu Tanzania tangu mwaka 2019. Ndugu Amanzi amezaliwa mwaka 1977. Kabla ya kupata Shahada yake ya Uzamili, ndugu Amanzi alipata Shahada ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2000-2003. Awali alikuwa Afisa Uendeshaji Muandamizi wa UTT Microfinance Plc kuanzia mwaka 2014 hadi 2018.Ndugu Amanzi pia alikuwa Meneja wa benki ya Akiba Commercial Plc tawi la Kariakoo kwa mwaka mmoja. Ndugu Amanzi ametumikia nafasi mbalimbali katika benki ya Akiba Commercial kama Msimamizi wa Mkopo Mwandamizi, Afisa mkopo wa shirika, Afisa Muuzaji na mtoa Huduma kwa Wateja.