Habari
MUWEKEZAJI KUTOKA INDIA
Katika kuendelea kufungua milango ya uwekezaji kwenye Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini, tarehe 22 Agosti, 2024 timu ya Wataalamu kutoka Bodi ikiongozwa na Meneja wa Kitengo cha Mipango na Masoko Bw. Goodluck Chuwa (kushoto) imekuta na muwekezaji kutoka nchini India Bw. Himanshu Dixit, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya eneo la uandaaji wa Filamu nchini.