emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

Muigizaji Bi. Hawa Ibrahim (Carolin) atembeliwa na Serikali hospitali


Tarehe 16 Julai, 2022 mara baada ya kumaliza sala maalum ya kumuaga aliyekuwa Muigizaji na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Wilaya ya Ilala Ndugu Juma Hamis Madenge, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo aliambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, kumjulia hali Muigizaji Bi. Hawa Ibrahim (Carolin) kufuatia kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Mama mzazi wa Muigizaji huyo aliishukuru Serikali kupitia Taasisi za Bodi ya Filamu na BASATA kwa kumtembelea Binti yake kwa kuwa kitendo hicho kinawapa faraja wanafamilia pamoja na mgonjwa.

Wengine walioambatana na Viongozi hao ni Makamu wa Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bi. Nyakwesi Mujaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Bw. Twiza Mbarouk, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Taifa (TDFAA) Bw. Salum Mchoma, pamoja na Watumishi kutoka Taasisi za Bodi ya Filamu na BASATA.

Tanzania Census 2022