emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

Kwaheri Ndugu Juma Hamis Madenge


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo akiwa amemwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, aliongozana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, ambapo kwa pamoja waliungana na ndugu, jamaa, marafiki, na Wadau wengine wa Filamu, katika sala maalum ya kumuaga aliyekuwa Muigizaji na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Wilaya ya Ilala Ndugu Juma Hamis Madenge, nyumbani kwake Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam.

Ndugu Madenge alifariki dunia Tarehe 15 Julai, 2022 ambapo atazikwa Tarehe 17 Julai, 2002 katika kijiji cha Mkundi, Mkoani Morogoro.

Tanzania Census 2022