emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ameendelea na utaratibu wa kutembelea wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ameendelea na utaratibu wa kutembelea wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza wakiwa katika mandhari mbalimbali za kazi ili kufahamu mazingira halisi ya utendaji wao.

Tarehe 14 Aprili, 2022 Dkt. Kilonzo aliwatembelea Watayarishaji wa Filamu "MEREMO" Kampuni ya Mroni Twins Entertainment Chanika jijini Dar es Salaam walipokuwa wakiendelea na utayarishaji wa kazi hiyo katika mandhari ya Hospitali ya Mama na Mtoto.

Filamu hiyo inaongozwa na Muongozaji Christina Mroni ambae pia ameshiriki kuigiza.

Tanzania Census 2022