emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI TANZANIA.


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo amekutana na Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania akiwemo Muandaaji wa Filamu kutoka nchini humo Bi. Gaelle Jones, lengo likiwa ni kupanga mikakati ya kushirikiana katika Programu mbalimbali za Bodi na zile zinazofanywa na Ubalozi huo nchini Tanzania ikiwemo utoaji wa mafunzo ya kuongeza weledi kwa wadau wa Filamu nchini.

Kikao hicho kimefanyika Oktoba 13, 2022 pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu Emmanuel Ndumukwa (TFB), Kaimu Meneja wa Utayarishaji Benson Mkenda (TFB), pamoja na Wawakilishi wengine wa Ubalozi akiwemo Sage Noukove na Kevin Theze.